Kampeini zaelekea kileleni Zimbabwe

Image caption Rais mstaafu wa Nigeria Olesegun Obasanjo yuko nchini Zimbabwe kama mwangalizi wa uchaguzi mkuu

Kampeini za kisiasa nchini Zimbabwe zinamalizika hii leo kabla ya uchaguzi mkuu hapo Jumatano wiki hii.

Kiongozi wa chama cha Movement for Democratic Change ambaye pia ni Waziri MKuu ,Morgan Tsvangirai, hii leo atahutubia mkutano wa hadhara mjini Harare katika uwanja alikofanya mkutano wake hio jana Rais Robert Mugabe.

Viongozi hao wawili wamekua katika serikali ya muungano tangu mwaka wa 2008 na wametofautiana kuhusu muda uliowekwa kufanyika uchaguzi. Kumekua pia na madai ya wizi wa kura, na vitisho dhidi ya wafuasi wa MDC.

Shirika la kimataifa linalotathmini hali ya mizozo The International Crisis Group limeonya kwamba hakuna mazingira ya uchaguzi huru na haki Zimbabwe.