'Jeshi lilirejesha demokrasia Misri' Kerry

Image caption Maandamano Misri

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry, amesema kuwa jeshi la Misri, lilikuwa linarejesha demokrasia nchini humowakati lilipomwondoa mamlakani aliyekuwa rais Mohammed Morsi mwezi jana.

Bwana Kerry alisema kuwa kuondolewa kwa Morsi, ilitokana na mambo ya mamilioni ya watu wa Misri .

Matamshi ya Kerry yanakuja huku polisi wakijiandaa kuwatawanya waandamanaji ambao ni wafuasi wa Morsi waliopiga kambi mjini Cairo.

Waziri wa mambo ya ndani wa Misri, ameahidi kuwa wafuasi wa Morsi, kuwa nguvu kaitatumika kubailiana nao ikiwa wataondoka kutoka eneo hilo kwa hiari.

Baraza la mawaziri la Misri liliamuru jeshi kumaliza maandamano hayo ambayo limeitaja kuwa tisho la usalama kwa nchi.

Licha ya kuombwa kuingilia mgogoro wa kisiasa Misri, Marekani imekataa kutaja hatua ya kumwondoa mamlakani Morsi kama mapinduzi ya kijeshi.

Kwa kufanya hivyo serikali ya Marekani itahitajika kusitisha msaada wake kwa taifa hilo wa dola bilioni moja nukta tano ambao hutolewa kila mwaka.

John Kerry ametoa kauli yake wakati wa mahojiano kwenye televisheini moja nchini Pakistan.

Wadadisi wanasema kuwa matamshi ya Kerry pia yatatafsiriwa kama uungwaji mkono wa serikali ya muda ya Misri.