Mtoto wa miaka 4 afa njaa Uingereza

Image caption Magdelena WOO-TCHAK na Marius KREZ-OH-WEK

Nchini Uingereza Mama na Baba wa kambo wa mvulana wa miaka minne aliyekufa njaa baada ya kufungiwa ndani ya chumba kimoja kwa miezi minne wamefungwa maisha jela kwa makosa ya kumuua mwanao.

Jaji aliyetoa hukumu hio amesema. Magdelena WOO-TCHAK na Marius KREZ-OH-WEK wanastahili kutumikia kifungo cha miaka 39 gerezani kabla ya kupatiwa nafasi ya kukata rufaa.

Wakati wa kesi hio daktari mmoja alisema mwili wa mtoto Daniel Pelka ulifanana na waathiriwa wanaofungiwa kwa jela bila chakula.

Kumekua na shutuma za umma kutaka kujua sababu za mtoto huyo kutookolewa licha ya mwili wake kupatikana na majeraha.

Wakati mmoja mtoto huyo alionekana akitafuta chakula kutoka kwa majaa ya taka. Wakati alipokufa mtoto huyo alikua na uzani wa kilo 10 ambao huwa ni uzani wa mtoto mchanga wa mwaka mmoja.