Sanamu za wakubwa zanyenyekewa

Sanamu za mawaziri wakuu wa zamani wa Uingereza katika bunge la nchi zitatengwa ili kuzuwia wale wabunge wanaogusa miguu ya sanamu hizo, wakiamini itawapa bahati.

Msimamizi aliiambia kamati ya bunge kwamba sanamu za viongozi kama Winston Churchill na Margaret Thatcher zinaharibika kwa sababu ya itikadi hiyo.

Ilani itawekwa, lakini mwenyekiti wa kamati amesema pengine vitawekwa vizuizi iwapo wabunge hawawezi kutuliza mikono yao.