Maafa India, baada ya Nyambizi kuzama

Image caption Nyambizi yazama nchini India bada ya Mlipuko

Habari kutoka Mumbai, India, zinasema kuwa waokoaji waliopiga mbizi kuwatafuta manusura hawajapata chochote. Mkuu wa jeshi la wanamaji nchini India D. K Joshi amesema kuwa watu 18 walikuwa kwenye nyambizi iliyozama baada ya kukumbwa na milipuko miwili mikubwa.

Waziri wa Ulinzi wa India A. K . Anthony ametaja tukio hilo kama baya zaidi kuwahi kutokea kwa wanamaji wa nchi hiyo. Iliwachukua wazima moto masaa kadhaa kuzima moto ambao ulionekana katika nyambizi.

Ripoti kutoka eneo la tukio hilo zinasema kuwa wanamaji kadhaa waliruka kutoka kwenye nyambizi kuokoa maisha yao baada ya mlipuko. Waliojeruhiwa wamepelekwa katika hospitali maalumu ya wanamaji. Maafisa wakuu wa idara ya wanamaji wamesema kuwa sehemu moja ya nyambizi hiyo ilikuwa imezama majini na eneo lingine kuchomeaka kabisa.

Nyambizi hiyo iliyotengenezewa Urusi ilifanyiwa marekebisho miezi mitatu iliyopita kwa gharama ya Dola Miloni 8.