Wakimbzi wa Syria wafurika nchini Iraq

Image caption maelfu ya wakimbizi kutoka Syria

Shirika la Umoja wa mataifa linaloshughulikia wakimbizi, UNHCR limesema kuwa idadi ya wakimbizi wanaotoka Syria kazkazini kuelekea nchini Iraq imeongezeka .

Msemaji wa shirika hiloAdrian Edwards, amesema kuwa maelfu ya wakimbizi wamevuka mpaka katika siku za hivi karibuni, wengi wao wakiwa wanawake, watoto na wazee.

Sababu ya ongezeko hilo hatahivyo haijulikani, lakini duru zinaarifu kwamba eneo hilo limekumbwa na makabiliano kati ya wapiganaji wa kiislamu na wale wa Kurd.

Wafanyikazi wa umoja wa mataifa wameshuhudia raia wengi wa Syria wakisafirishwa kwa mabasi. Baadaye raia hao huvuka kuingia nchini Iraq kwa kutumia daraja.

Msemaji huyo amesema kuwa zaidi ya wakimbizi miilioni 1.9 raia wa syria wamekimbia vita wengi wao wakielekea lebanon,Jordan na Uturuki.