Bo Xilai akejeli shahidi

Bo Xilai mahakamani katika jimbo la Shandong

Katika siku ya tatu ya kesi ya mwanasiasa mashuhuri wa Uchina, Bo Xilai, mshtakiwa ameutoa maanani ushahidi dhidi yake kuhusu madai ya ufisadi yanayomkabili.

Shahidi mmoja amesema alimuona Bwana Bo akimwambia mkewe achukue hongo ya dola 800,000 kutoka mradi wa majenzi wa mji wa Dalian, ambako mwanasiasa huyo aliwahi kuwa meya.

Lakini Bo alisema kuwa ni mtu mpumbavu pekee anayezungumza swala la rushwa mbele ya mashahidi.

Maelezo ya kesi hiyo yanaendelea kuwekwa katika mtandao wa Weibo nchini humo.

Mwandishi wa BBC anasema inachukuliwa kuwa Bwana Bo atapatikana na hatia, kwa sababu umaarufu wake na hamu yake ya madaraka ukitishia viongozi wenzake wa chama cha kikoministi.

Mahakama hiyo bado haijaangazia shtaka la utumizi mbaya wa wadhifa.

Bwana Bo ameshtakiwa kwa kufunika kuhusika kwa mkewe katika mauaji ya mfanyabiashara mmoja kutoka Uingereza.