Wayahudi 450 wa Ethipioa warejeshwa Israel

Image caption Wayahudi wenye asili ya Ethiopian wakiandamana nje ya bunge la Israel

Raia 450 wa Ethiopia, wenye asili ya Kiyahudi wamesafirishwa hadi Israel na hivyo kumaliza mpango wa serikali ya Israel wa kuwarejesha nyumbani raia wake waliokuwa nchini Ethiopia.

Waziri wa Uhamiaji wa Israel, Sofa Landver, amenukuliwa akisema kuwa shughuli hiyo imekuwa ya kihistoria.

Idadi kubwa ya watu wa jamii ya Falash Mura wamekuwa wakiishi katika hali ya umasikini mkubwa Kaskazini mwa Ethiopia.

Mababu wa jamii hiyo ya Falash Mura, walijiunga na dini ya Kikristo kufuatia shinikizo karne ya kumi na tisa.

Jamii hiyo imekuwa ikishinikiza serikali ya Israel kuwapa idhini ya kuishi nchini humo.

Kampeini hiyo hata hivyo umekumbwa na utata, huku waisraeli kadhaa wakihoji uhusiano wao na wayahudi wengine na wengine wakishutumu serikali ya nchi hiyo kwa kutoa msaada kwa jamii hiyo.

Mwaka wa 2010, serikali ya Israel, ilikubali kuanzisha upya mpango wake wa kuwarejesha nyumbani raia wake waliokuwa wakiishini nchini Ethiopia, mpango ambao ulisitishwa mwaka wa 2008.

Wahamiaji mia nne hamsini wamekuwa wakiishi katika kambi za muda mjini Gondar, Kaskazini mwa Ethiopia wakisubiri kusafirisha hadi Israel.

Kundi hilo ndilo la mwisho kwa raia elfu nane wa Ethiopia ambao walitimza masharti ya kusafirishwa hadi nchini Israel.

Wayahudi hao walisafirishwa kwa ndege mbili zilizokodiwa hadi uwanja wa ndege wa Gurion na kulakiwa na jamaa zao waliokuwa nchini Israel.

Kwa mujibu wa gazeti la The Times la Israel, wanachama elfu kumi na mbili wa jamii hiyo ya Falash nchini Ethiopia hawakuruhusiwa kuhamia nchini Israel.

Tangu mwaka wa 1948, Takriban Wayahudi elfu tisini nchini Ethiopia wamesafirishwa hadi nchini Israel.

Kwa sasa jamii hiyo ndio masikini zaidi nchini Israel.