Akufo-Addo apoteza kesi dhidi ya Mahama

Image caption Kiongozi wa upinzani nchini Ghana Nana Akufo-Addo

Mahakama ya rufaa nchini Ghana imemthibitisha rais John Dramani Mahama kuwa mshindi wa uchaguzi wa Urais uliofanyika Desemba mwaka uliopita.

Baada ya kusikiliza rufaa iliyowasilishwa na chama kilichoshindwa cha New Patriotic Party, NPP, mahakama hiyo ilifutilia mbali kesi hiyo iliyowasilishwa na upinzani.

Mgombea wake wa urais Nana Akufo-Addo, ambaye alishindwa na idadi ndogo sana ya kura na rais Mahakama, alidai kulikuwepo na ulaghai mwingi wakati wa kupiga kura na hivyo kuiomba mahakama kufutilia mbali matokeo yake.

Taifa la Ghana linakisiwa kuwa nchi iliyokomaa kidemokrasia katika kanda ya Afrika Magharibi na imeandaa uchaguzi huru wa vyama vingi mara sita katika kipindi cha miaka ishirini iliyopita.