Raia wawili wa Rwanda wauawa Gesenyi

Image caption Ramani ya Rwanda

Wanawake wawili wa Rwanda wameuawa katika shambulio la kombora lililoangukia upande wa Rwanda unaopakana na nchi ya Jamuhuri ya kidemokrasi ya kongo.

Tukio hilo limetokea katika mji wa Rwanda wa Gisenyi.

Rwanda imeishutumu jeshi la Congo kwa kurusha kombora hilo.

Vikosi vya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo vinapambana na waasi wa M23 wanaoaminiwa kusaidiwa na Rwanda.

Serikali ya Rwanda imekuwa ikimanusha madai hayo.