Chama cha Tony Abbot chashinda Australia

Tony Abbott na familia yake wakipiga kura

Chama cha Australia cha Liberal-National kimeshinda katika uchaguzi mkuu.

Katika hotuba yake ya kukubali ushindi, kiongozi wa chama hicho, Tony Abbott, aliwaambia wafuasi kwamba ataunda serikali ya kuaminika na yenye uwezo wa utendaji.

Alisema baada ya mwaka kodi ya uchafuzi wa mazingira itafutwa, mashua zinazopeleka wakimbizi Australia kutoka Asia zitakuwa hazipo, na bajeti itakaribia kuwa na ziada.

Alipokiri kushindwa, kiongozi wa chama cha Labor, Kevin Rudd, alisema kuwa alimpigia simu Bwana Abbot kuitakia mema serikali mpya kwa changamoto kubwa inazokabili.

Aliwaambia wafuasi wake kwamba atajiuzulu kama kiongozi wa chama.