Australia yamaliza kupiga kura

Wapihaji kura wa Australia wasubiri kwenye foleni

Raia wa Australia wamemaliza kupiga kura katika uchaguzi mkuu ambapo waziri mkuu wa chama cha Labor, Kevin Rudd, anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Tonny Abbott.

Kura za maoni za hivi karibuni zinaonesha Bwana Abbot na chama chake cha Liberal-National akiongoza, lakini wanasiasa wote wawili wanasema matokeo hayatabiriki na waliwaomba wafuasi wao wapige kura.

Foleni zilikuwa ndefu katika vituo vya kupiga kura - katika sheria ya Australia kupiga kura ni lazima kwa kila mtu zaidi ya umri wa miaka 18.

Maswala muhimu katika kampeni yalikuwa uchumi, wahamiaji na kodi juu ya uchafuzi wa mazingira.

Lakini katika kampeni wanasiasa wenyewe ndio walikuwa muhimu kushinda mjadala.