60 wauawa kwenye mapigano CAR

Image caption Waasi wa Seleka

Takriban watu 60 wameuawa kwenye mapigano katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati, kati ya waasi na wapiganaji wanaomuunga mkono rais aliyendolewa mamlakani mwezi Machi.

Msemaji wa rais alielezea kuwa wapiganaji wanaomuunga mkono Francois Bozize walivamia vijiji katika eneo la Kaskazini Magharibi mwa mji mkuu.

Haya ndiyo mashambulizi ya kwanza makubwa kufanywa na majeshi ya rais aliyeondolewa mamlakani mwezi Machi.

Umoja wa Mataifa umeonya kuwa Jamuhuri nya Afrika ya Kati huenda ikaporomoka na hivyo kutishia usalama wa eneo zima.

Taifa hilo lina madini ya dhahabu na almasi ingawa imekuwa na misukosuko tangu kujipatia uhuru wake

Michel Djotodia, kiongozi wa uliokuwa muungano wa waasi wa Seleka aliyeapishwa kama rais mapema mwezi huu ameahidi kuondoka mamlakani baada ya uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka 2016