Serena Williams ashinda US Open tena

Image caption Williams ashinda kwa mara ya 17

Bingwa wa dunia wa Tenis kwa wanawake, Serena Williams ameshinda kwa mara ya tano shindano la US Open, na kuwa shindano lake la kubwa la 17 kulishinda katika fainali lliyokuwa yenye mbwembwe dhidi ya Victoria Azarenka katika uwanja wa Flushing Meadows.

Serena mwenye umri wa miaka 31, aliweza kuibuka mshindi dhidi ya Azarenka kwa kumshinda kwa seti tatu kati ya nne na hivyo kupata ushindi kwa mara nyingine.

Williams sasa ameshinda shindano hilo kwa mara ya kumi na saba.

Lakini baada ya ushindani mkali kutoka kwa Azarenka, Williams alilazimika kujitahidi zaidi ya alivyokuwa anacheza ili aweweze kupata ushindi kama ilivyokuwa katika michezo mingine 16 iliyopita ambapo aliweza kushinda.

Azarenka, mwenye umri wa miaka 24, aliwahi kumshinda Williams mara mbili mwaka huu , mara ya mwisho kwenye mchezo uliochezwa wa kirafiki eneo la Cincinnati mkesha wa shindano la US Open, mwaka huu na kujiamini kuwa angeweza kumshinda mmarekani kwenye ukumbi mkubwa.

Williams alionekana kuwa katika hali nzuri wakati wa shindano lote.