Mmarekani mpigania Al shabaab auawa

Image caption Amriki

Wakaazi wa eneo la Gedo Kusini Magharibi mwa Somalia, wanasema kuwa mwanamgambo wa kiisilamu mwenye asili ya kimarekani, ameuawa na wanamgambo wa al Shabaab.

Duru zinasema kuwa aliuawa baada ya kuvamiwa na wanamgambo wenzake katika eneo alilokuwa anaishi.

Mmarekani huyo anayejulikana kwa jina lake Abu Mansoor al Amriki au Omar Hammami, aliuawa pamoja na mwenzake Usama al-Britani, raia wa Pakistan mwenye asili ya Uingereza.

Inaarifiwa wawili hao walikuwa wamejitenga na kundi la Al Shabaab . Mwenzao mwenye asili ya Misri alikamatwa.

Kundi la Al Shabaab limekuwa likikumbwa na migawanyiko huku wapiganaji wa kigeni pamoja na wapiganaji wengine wakilengwa na kiongozi wa mwenye msimamo mkali wa Al shabaab Ahmed Abdi Godane.

Godane anaongoza wapiganaji wake katika kupigania wanachokiita taifa la kiisilamu.