Wanawake waongezeka bungeni Rwanda

Image caption Wanawake na wanaume wana nafasi sawa za kushikilia katika taasisi za serikali kwa mujibu wa katiba

Idadi ya wanawake waliochaguliwa katika bunge la Rwanda imepanda kutoka asilimia 56 hadi 64 katika bunge lenye wabunge 80. Hii ina maanisha idadi yao ni wanawake 51 kati ya wabunge 80 walioko katika bunge la waakilishi.

Hayo yamebainika baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa wabunge uliomalizika Jumatano.

Idadi hii inaendelea kuifanya Rwanda kuwa miongoni mwa mataifa yenye wanawake wengi bungeni.

Rwanda iliweza kufikia hilo mara ya kwanza katika uchaguzi wa mwaka 2008 wakati wanawake, waliposhinda asilimia 56 ya viti katika bunge la waakilishi.

Kando na nafasi 24 zilizoachiwa wanawake katika bunge hilo, ambazo ziliamuliwa tarehe 17 Septemba, wanawake pia walishinda nafasi zengine 26 kati ya 53 zilizokuwa zinawaniwa.

Waangalizi wanasema kuwa wanawake wanafanya vyema kwenye uchaguzi huo wa bunge kwa sababu ya nafasi wanazopewa katika uchaguzi wa vyama vya kisiasa, kinyume na ilivyokuwa siku za nyuma ambapo ni wanaume pekee waliokuwa katika msitari wa mbele kugombea nafasi za kisiasa.

Mfano wakati wa uchaguzi wa mashinani wa chama tawala cha (RPF) kiliamuru kuwa wapiga kura wachague wanawake na wanaume.

Na kisha wagombea wote wa kike na wa kiume waliwekewa nafasi sawa za kuwania katika chama.

Lakini habari hizi hazisherehekewi na kila mtu. Baadhi ya wanaume wanalalamika wakisema kuwa ongezeko la wanawake kushikilia nyadhifa za kisiasa, linatishia kazi yao ngumu katika miaka ya hivi karibuni.

Katiba ya mwaka 2003 inasema kuwa mtu wanwake na wanume wanaweza kushikilia asilimia 30 au zaidi ya taasisi zote za maamuzi serikalini

Katika bunge la senate, wanawake wanashikilia nafasi 10 kati ya 25 zilizopo