30 wauawa na magaidi Nairobi, Kenya

Image caption Majeruhi katka kisa cha uvamizi wa duka la ghorfa nne Nairobi.

Kufuatia watu wenye silaha kuvamia jengo la ghorofa nne lenye maduka la Westgate jijini Nairobi sasa inahofiwa angalu watu 30 wameuawa na wengine zaidi ya hamsini kujeruhiwa vibaya.

Kwa mujibu wa taarifa za Shirika la Msalaba mwekunde la Kenya idadi ya waliofariki imeongezeka hadi 30. Washambulizi wangali ndani ya jengo hilo na inaaminika wangali wamewateka nyara baadhi ya watu waliokuwa katika duka hilo.

Wakati huo huo taarifa kutoka ikulu ya Rais Kenya inasema kwamba serikali imeanzisha oparesheni kali ya uokozi.

Hii nikutokana na taarifa kwamba watu hao wenye silaha wanawashikilia mateka watu kadhaa ndani ya jengo hilo.

Mtu mmoja ambaye amejificha ndani ya jengo hilo ameiambia BBC kwamba ameona watu wapatao 36 wakiwa wameshikwa mateka na waru hao.

Hata hivyo Ikulu ya Kenya imesema ni mapema sana kusema kwamba tukio hilo ni la kigaidi.

Ikulu ya Nairobi vilevile imesema ni mapema mno kusema kama uvamizi huo ni tukio la kigaidi au la.

Walioshuhudia kisa hicho wanasema watu waliovalia magwanda yalioonekana kama ya kijeshi huku wengine wakiwa wamefunika nyuso zao walivamia jengo hilo kwa wakifyatua risasi.

Kisa hicho kimetokea katika eneo la kifahari la Westland jijini Nairobi .

Image caption Jengo la Duka lililovamia wa watu wenye silaha

Maduka hayo ya Westgate hupendelewa sana na watu matajiri na wageni.

Walioshuhudia tukio hilo, wanasema kuwa maguruneti piya yalitumika.

Polisi waliojihami kwa silaha wamezingira jengo la maduka liitwalo Westgate, katika mtaa wa Westlands, na kuna taarifa ya watu waliojeruhiwa wakitolewa hapo kwa machera.

Hadi sasa kuna watu ambao idadi yao haijulikani wamo ndani ya jengo hilo.

Wakati huo huo Hospitali ya Aga Khan, ya Nairobi imetoa ujumbe wa dharura kwamba damu inatakikana kwa haraka.

Hii ni kutokana na taarifa kwamba kuna idadi kubwa ya majeruhi ambao wamepelekwa katka hospitali hiyo.