Afghanistan yafurahi Taliban afunguliwa

Mullah Baradar

Wakuu wa Pakistan wanasema wamemuachilia huru mfungwa mwenye cheo katika kundi la Taliban - Mullah Abdul Ghani Baradar - ili kurahisisha juhudi za mapatano nchini Afghanistan.

Serikali ya Afghanistan imekaribisha habari hizo na inamuona Mullah Baradar kuwa mmoja kati ya maafisa waandamizi walio tayari kuzungumza.

Afisa mmoja wa Afghanistan alimuelezea Mullah Baradar - naibu kiongozi wa zamani wa Taliban - kuwa mjumbe wa amani.

Hata hivyo, waandishi wa habari wanasema haijulikani Mullah Baradar ana kauli gani bado katika kundi hilo la wapiganaji.

Alikamatwa mjini Karachi, Pakistan, mwaka wa 2010.