Wachunguzi wa UN kurejea Syria

Image caption Viongozi wa dunia wamekuwa akitofautiana kujhusu hatua za kuchukua dhidi ya Serikali ya Assad kwa kutumia silaha za kemikali dhidi ya raia

Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa wanajiandaa kurejea nchini Syria kuendelea na uchunguzi kuhusu ikiwa silaha za kemikali zilitumika katika miji mingine ya nchi hiyo mbali na Damascus

Wachunguzi hao tayari wamethibitisha kuwa gesi ya sumu aina ya Sarin, ilitumika katika kuwashambulia watu katika kitongoji kimoja cha Damascus mwezi Agosti tarehe 21 ambapo mamia waliuawa.

Sasa wanajiandaa kutembelea maeneo mengine matatu ambako inaaminika silaha za sumu zilitumika ingawa kwa kiwango kidogo mapema mwaka huu. Shambulizi lilifanyika katika eneo la Aleppo,mjini Homs na karibu na Damascus.

Serikali ya Syria pamoja na waasi zinatuhumiana kwa kufanya mashambulizi .Wachunguzi hao wataamua ikiwa silaha za kemikali zilitumika lakini hawatasema ni nani wa kulaumiwa.