Wanafunzi washambuliwa chuoni Nigeria

Ramani ya Nigeria

Jeshi la Nigeria linasema watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Kiislamu wa kundi la Boko Haram wameshambulia wanafunzi waliolala katika chuo cha kilimo katika jimbo la Yobe, kaskazini mwa nchi.

Inaarifiwa kuwa wapiganaji waliwafyatulia risasi wanafunzi wa chuo hicho katika eneo la mashambani la Gujba.

Inaarifiwa piya kuwa walichoma moto madarasa .

Duru za hospitali kaskazini-magharibi mwa Nigeria zinasema watu baina ya 40 hadi 50 wameuwawa katika shambulio hilo.