Kimbunga Phailin chapiga Orissa, India

Wavuvi wa India wametakiwa waondoke mwambao wa Orissa kabla ya kimbunga kufika

Kimoja kati ya vimbunga vikubwa kabisa kuipiga India kimefika bara, kikivuma na upepo wa kasi ya kilomita 200 kwa saa.

Kimbunga Phailin kinapita katika jimbo la Orissa; watu zaidi ya nusu milioni wa huko na jimbo la Andhra Pradesh wamehamishwa na kupelekwa maeneo salama.

Usafiri umetatanika sana.

Lakini wakuu wanasema safari hii wamejitayarisha vema zaidi kushinda mwaka wa 1999, ambapo kimbunga kikubwa kiliuwa watu zaidi ya 10,000 katika jimbo la Orissa.