India yahisabu hasara baada ya kimbunga

Kimbunga Phailin kikipiga Orissa na Andhra Pardesh

Maafisa wa India wanaoshughulika na kazi za uokozi wameanza shughuli zao baada ya Kimbunga Phailin kupiga majimbo ya mashariki na kusababisha mafuriko kwenye miji na vijiji.

Wakuu wanasema wasaidizi wametumwa maeneo yaliyopigwa na kimbunga katika majimbo ya Orissa na Andhra Pardesh, kuwaokoa wale wanaofikiriwa wamenasa chini ya vifusi.

Miti iliyoporomoka imeuwa kama watu saba.

Lakini waandishi wa habari wanasema matayarisho na operesheni kubwa iliyofanywa ya kuwahamisha watu kabla ya kimbunga, imenusuru maisha.

Uharibifu uliotokea bado haujulikani kwa ukamilifu na waya za umeme na mawasiliano zimekatika katika maeneo mengi.

Kimbunga cha mwaka 1999 kiliuwa watu 10,000 katika jimbo la Orissa.