30 wafa kwa tetemeko Ufilipino

Image caption Baadhi ya majengo yaliyodondoka baada ya kupigwa na tetemeko Philippines

Zaidi ya watu 30 wameripotiwa kufa baada ya tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa vipimo vya 7.2 kupiga katikati ya Philippines.

Idara ya giologia ya Marekani imesema tetemeko hilo limepiga chini ya kisiwa cha Bohol kinachojulikana kuwa na fukwe zenye mchanga.

Wengi wamefariki baada ya majengo kudondoka katika eneo la Bohol karibu na jimbo la Cebu. Majengo mengi na makanisa yameharibiwa kwa tetemeko hilo.

Tetemeko hilo limepiga majira ya saa mbili kwa saa za Philipine ambapo pia ni siku ya mapumziko.

Maafaisa wanasema karibu watu 16 wamethibitishwa kufariki katika eneo la Bohol na 15 katika eneo la Cebu mji wa pili kwa ukubwa nchini Philipines. Mtu mmoja amefariki karibu na kisiwa cha Siquijor huku wengine kadhaa wakijeruhiwa.