Amnesty:Marekani inakiuka sheria za vita

Image caption Mwanawe Mohammed alifariki kwenye mashambulizi ya kutumia ndege wasio na rubani

Mashambulizi ya kutumia ndege wasio na rubani ambao hufanywa na shirika la CIA la Marekani yamesemekana kusababisha mauaji kinyume na sheria baadhi yanayoweza kusemekana kuwa uhalifu wa kivita.

Hii ni kwa mujibu wa shirika la kimataifa la Amnesty International.

Shirika hilo linasema kuwa limedurusu mashambulizi tisa yaliyofanywa kwa kutumia ndege wasiokuwa na rubani Kaskazini mwa Waziristan na kugundua kuwa idadi kubwa ya waathiriwa hawaku wamejihami.

Katika ripoti nyengine kuhusu mashambulizi sita yaliyofanywa kwa kutumia ndege hizo, shirika la Human Rights Watch limesema kuwa wawili kati ya waliouawa walikuwa raia wasio na hatia jambo linalokiuka sheria za kimataifa.

Utumizi wa ndege zisizo na silaha kufanya mashambulizi limekuwa jambo ma kawaida kwa Marekani katika vita vyake dhidi ya wapiganai wa kiisilamu.

Kuna taarifa chache sana kuhusu matumizi ya ndege hizo.

Maafisa wakuu wa Al Qaeda na Taliban, wameuawa kwenye mashambulizi kwa kutumia ndege hizo nchini Pakitsna , lakini raia wasio na hatia pia wameuawa.

Mashambulizi hayo yamesababisha ghadhabu nchini Pakistan ambako wengi wanahisi kuwa yanasababisha vifo kiholela na kuwajeruhi watu wasio na hatia.

Wiki jana , wachunguzi wa Umoja wa Mataifa, waligundua kuwa raia wasiopungua 400 waliuawa nchini Pakistan, idadi hiyo ikiwa juu zaidi ya idadi ambayo ishawahi kukubaliwa na Marekani.

Mjumbe maalum wa UN Ben Emmerson aliituhumu Marekani kwa kukiuka masharti na sheria za kimataifa kwa kutumia nguvu nje ya mameneo ya vita.

Kuweza kujua idadi kamili ya watu waliofariki au kujeruhiwa kwenye mashambulizi kama hayo huwa vigumu kwani vyombo binafsi vya habari huzuiwa kwenda katika maeneo hayo.