Mkutano muhimu kuhusu Syria kufanyika London

Image caption Hlai nchini Syria inaendelea kuwa mbaya mno upinzani ukisema hautaki mazungumzo na Assad

Nchi za kiarabu pamoja na mawaziri wa nchi za kigeni wa mataifa ya Magharibi, wanakutana hii leo mjini London na maafisa wa upinzani wa Syria katika juhudi za kuwashawishi kuhudhuria mkutano wa amani utakaofanyika hivi karibuni.

Kikundi muhimu cha wanachama wa upinzani rasmi kinatishia kususia mazungumzo hayo yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujao mjini Geneva.

Baraza la upinzani la Syria limekuwa likikataa kushiriki mazungumzo na waakilishi wa serikali ya Rais Bashar al-Assad.

Mawaziri wanatarajiwa kueleza umuhimu wa ushirikiano kati ya makundi ya upinzani ikiwa mazungumzo ya amani yatafanikiwa.

Mjini London, mawaziri wa mambo ya kigeni kutoka katika nchi 11 zinazijiita marafiki wa Syria, zitajaribu kubuni agenda ya mkutano wa pili wa Geneva.

Ufaransa, Italy, Qatar, Saudi Arabia, Uturuki na Milki za kiarabu, zinatarajiwa kusisitiza kuwa mkutano huo sharti uwe kuhusu kipindi cha mpito kisiasa nchini Syria pasina serikali ya Assad

Akiongea kabla ya mkutano huo wa London, waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry alisisitiza kuwa upinzani wa Syria kamwe hauwezi kukubali Rais Assad kusalia madarakani.

‘‘Ikiwa anadhani kuwa anaweza kusuluhisha mgogoro huo kwa kugombea Urais, naweza nikamwambia kuwa wazi kuwa vita hivi havitakwisha,’’ alisema bwana Kerry babada ya mazungumzo yake na mataifa wanachama wa muunganowa nchi za kiarabu.