Merkel: Majasusi wamedakua simu zangu

Image caption Chansela wa Ujerumani Angela Merkel

Chansela wa Ujerumani Angela Merkel amempigia simu Rais wa Marekani Barak Obama baada ya kupata taarifa kuwa Idara ya Ujasusi ya Marekani imekuwa ikifanya udakuzi wa mawasiliano ya simu zake za mkononi.

Msemaji wa serikali ya Ujerumani, Steffen Seibert amesema serikali ya Ujerumani inahitaji uthibitisho wa taarifa hizo na kusema kwamba kitendo hicho ni uvunjifu wa uaminifu.

Naye msemaji wa ikulu ya White House, Jay Carney amewaambia waandishi wa habari kwamba, Bw. Obama amemhakikishia Bi. Merkel kwamba, Marekani haikuwahi kusikiliza mawasiliano ya simu zake na haitafanya hivyo wala kwa siku za usoni japo haikufafanua kama mawasiliano Bi Merkel yaliyahi kufuatiliwa.

Wakati huo Umoja wa Ulaya unaanza mkutano wake mjini Brussels nchini Ubelgiji huku kukiwa na malalamiko kuhusu majasusi wa Marekani kudaiwa kuingilia mawasiliano ya simu.