Wanawake na wamaune karibu kuwa sawa

Pengo la kijinsia linapungua

Pengo kati ya wanaume na wanawake limepungua kwa kiasi tu katika kipindi cha mwaka mmoja. Hii ni kwa mujibu wa taarifa ya kongamano la kimataifa la kiuchumi{World Economic Forum- WEF}.

Nchi za Iceland, Finland na Norway zinaongoza orodha ya mataifa 136 ambapo kumekuwepo na usawa kati ya wanawake na wanaume katika nyanja ya elimu, uchumi na afya.Mashariki ya kati na Kaskazini mwa Afrika yametajwa kama maeneo ambapo hali ingali mbaya kwa wanawake katika kupata nafasi za uwongozi, elimu na afya bora.

Nchi za Ufilipino na Nicaragua ziko kwenye kumi bora.Kongamano la WEF limekuwa likitoa taarifa yake kwa miaka minane sasa. Ripoti hii inajiri wakati BBC imekuwa na mwezi mmoja ulioangazia masuala ya wanawake hususan nafasi yao katika jamii.