Radio Shebelle yafungwa Mogadishu

Msikilizaji wa redio Somalia

Polisi nchini Somalia wamevamia makao makuu ya shirika la redio la Shebeelle, mjini Mogadishu, na hivo kukata matangazo yake.

Polisi walidai kuwa kituo hicho cha redio kilikuwa kinatumia jengo la serikali kinyume na sheria.

Askari waliokuwa na silaha walizingira kituo hicho kilioko karibu na uwanja wa ndege wa Mogadishu, na kuwakamata waandishi wa habari.

Siku nne zilizopita wizara ya mambo ya ndani ya nchi iliitaka redio Shebelle ilihame jengo.

Wakuu walisema wanalichukua tena jengo hilo ambalo ni la serikali.

Waandishi wa habari wa redio Shebelle walikuwa wakitangaza habari kuhusu operesheni hiyo wakati jengo linavamiwa, kabla ya jengo kufungwa kabisa.

Waandishi wa habari 6 wameuwawa nchini Somalia mwaka huu