AU yazuwiliwa kufika Abyei

Abyei, Sudan

Umoja wa Afrika umeishutumu serikali ya Sudan kuwa inauzuwia ujumbe wa AU kuzuru Abyei, eneo lenye mafuta ambalo linaaniwa na Sudan na Sudan Kusini.

Taarifa ya AU inasema ziara hiyo imeakhirishwa mara mbili katika juma, kwa sababu za usalama ambazo zinaonesha siyo sababu nzito.

Umoja wa Afrika unajaribu kupatanisha baina ya nchi hizo mbili kuhusu swala la Abyei, ambalo halikupatiwa ufumbuzi tangu Sudan Kusini ilipojitenga kutoka Sudan mwaka wa 2011.