Rwanda yanga'aa katika biashara

Image caption Ukarabati wa miundo msingi umepewa kipaombele Rwanda

Benki ya dunia katika utafiti wake kuhusu urahisi wa kufanya biashara kote duniani, inaonyesha kasi ya mageuzi ya kisheria katika sekta ya biashara, ambayo inasema ndio njia muhimu sana ya kukuza uchumi.

Ripoti hiyo inasema kuwa Rwanda, Urusi na Ufilipino ni miongoni mwa nchi ambazo zimeboresha sheria na vikwazo vya kufanya biashara ili kuimarisha hali na mazingira ya biashara na kuwapa msukumo vijana kutaka kujiingiza katika biashara na uchumi.

Aidha ripoti hiyo inasema kuwa takriban nusu ya nchi ishirini ambazo zimeongeza kasi na mazingira ya biashara ziko barani Afrika.

Ripoti hiyo pia inaelezea kuwa nchi zilizo na vikwazo vichache vya kibiashara kuhusu wanawake pia zimefanya vyema katika kuimarika kibiashara.