Waasi wa M23 watimuliwa Bunagana

Image caption Wanajeshi wa DRC wiki hii wamefanikiwa kukomboa maeneo mengine kutoka kwa M23

Wanajeshi wa DRC wamefanikiwa kuwatimua waasi wa M23 kutoka katika ngome yao kuu katika eneo la Bunagana.

Wanajeshi hao wamekomboa mji wa Bunagana kufuatia makabiliano makali adhuhuri ya leo ambapo baadhi ya waasi walilazimika kuimbilia msituni huku baadhi wakidai waliingia Uganda baada ya kuvalia mavazi ya kiraia.

Msemaji wa serikali alisema kuwa mji wa Bunagana ulio katika mpaka wa Uganda na DRC, sasa uko chini ya wanajeshi wa serikali.

Wenyeji wa mji huo walithibitishia BBC kuwa mji huo ulikombolewa na kuwa waasi wamekuwa wakitoroka mapambano makali dhidi yao.

Hatua hii ya wanajeshi ni sehemu ya ushindi mkubwa ambao wanajeshi wamekuwa wakiupata dhidi ya waasi hao wa M23 walianza harakati zao dhidi ya serikali ya Congo mwaka jana wakidaiwa kusaidiwa na serikali ya Rwanda.

Mnamo siku ya Jumatatu mjumbe maalum wa M23 hawana tena nguvu za kijeshi kwani sio tesho tena.,

Umoja wa Mataifa umesema kuwa wakimbizi elfu tano wamelazimika kutoroka Bunagana na kuingia Uganda kwa usalama wao.