Abyei wapiga kura kujiunga na S. Kusini

Image caption Wasichana wa Kabila la Ngok Dinka katika jimbo la Abyei

Wananchi wa jimbo lenye mzozo la Abyei wamepiga kura ya kujiunga na Sudan Kusini katika kura isiyo rasmi ya maoni iliyopigwa na kabila moja kati makabila makuu mawili ya nchi hiyo.

Msemaji wa Kamati inayosimamia kura hiyo ya maoni amesema asilimia 98.9 ya waliopiga kura kutoka kabila la Ngok Dinka wamepiga kura ya kukubali kuijiunga na Sudan Kusini.

Wanachama wa Arab Misseriya ambao wana mshikamano na Sudan wamekataa kupiga kura hiyo na kusema hawatatambua matokeo hayo.

Umoja wa Afrika umeelezea kura hiyo maoni kuwa tishio la amani kati Sudan na Sudan Kusini.