AU yaomboleza waliozama Lampedusa

Wahamiaji Lampedusa

Umoja wa Afrika umetangaza kuwa Jumapili ni siku ya maombolezo katika bara zima, kwa wale waliokufa katika ajali ya meli katika bahari ya Mediterranean nje ya Lampedusa mwezi kamili uliopita.

Wahamaji zaidi ya 350, wengie wao wanafikiriwa kutoka Somalia, Eritrea na Syria, walizama katika maafa hayo wakijaribu kufika Ulaya.

Umoja wa Afrika umetoa wito kwa nchi wanachama kuwasalia waliokufa na kupepea bendera za taifa nusu mlingoti.

AU imesema maafa hayo yanafaa kukumbusha mataifa kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa tatizo hilo.