Wapinga kuahirishwa kesi ya Kenyatta

Image caption Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya

Waathirika wa kesi inayomkabili rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta wameutaka Umoja wa Mataifa kukataa wito wa kutaka kucheleweshwa kwa kesi dhidi ya Rais Kenyatta katika mahakama ya kimataifa ya ICC mjini The Hague, Uholanzi.

Baadhi ya viongozi wa Afrika wameandaa rasimu ya azimio la kuomba kesi inayomkabili Rais Kenyatta iahirishwe kwa mwaka mmoja kwa masilahi ya usalama wa taifa, kufuatia shambulio la kigaidi katika kituo cha kibiashara cha Westgate mjini Nairobi.

Lakini mwanasheria wa waathirika, Fergal Gaynor, amesema kucheleweshwa kwa kesi kutapunguza nafasi ya kupatikana haki kwa waathirika. Bwana Kenyatta anakanusha mashitaka yanayomkabili dhidi ya uhalifu wa kibinadamu, kufuatia ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa 2007.