Mshukiwa aliyemuua Mnigeria India akamatwa

Image caption Polisi wa Goa

Polisi katika jimbo la Goa nchini India wamesema kuwa wamemkamata mtu mmoja anayehusishwa na mauaji ya raia mmoja wa Nigeria juma lililopita ambayo yalizua maandamano makubwa kutoka kwa raia wa Nigeria katika jmbo hilo.

Katika maandamano hayo polisi walifanikiwa kuwatia mbaroni raia wa Nigeria ambao walikuwa wamefunga barabara moja kubwa kwa masaa kadhaa.

Mjumbe wa Nigeria nchini humo amesema anahofia usalama wa raia wa Nigeria katika jimbo la Goa huku akitaja hatua ya kuwakamata wananchi hao wa Nigeria kama uchochezi.

Waziri mmoja katika jimbo la Goa awali alikuwa ameelezea kuwa idadi ya raia 40,000 inayoishi nchini Nigeria ni kama saratani.

Maafisa wa polisi wamedai kuwa mauaji ya raia huyo wa Nigeria yanatokana na uhasama uliopo kati ya walanguzi wa mihadarati nchini humo na wenzao wa kutoka Nigeria.