Uharibifu wa Kimbunga Haiyan Ufilipino

Image caption Maelfu ya watu wamefariki kutokana na kimbunga Haiyan nchini Ufilipino

Mkuu wa shirika la msalaba mwekundu nchini Ufilipino ametaja uharibifu uliotokana na kimbunga Haiyan, kuwa mbaya sana.

Maafisa wanakadiria watu 10,000 wamefariki mjini Tacloban na kwingineko.Mamia ya wengine wamepoteza makao yao.

Juhudi za uokozi zinaendelea, ingawa zimetatizwa kutokana na barabara na viwanja vya ndege kuharibiwa vibaya.

Kimbunga hicho kimepiga Kaskazini mwa Vietnam karibu na mpaka na China , ingawa kasi yake imepungua.

Moja ya vimbunga vibaya zaidi kuwahi kutokea katika historia ya Ufilipino, Haiyan, kilivuka na kupiga eneo la Mashariki mwa Pwani mwa Leytena mnamo siku ya Ijumaa.

Kimbunga hicho kimepiga visiwa sita katika eneo la Kati mwa Ufilipino.

Maafisa wanakadiria watu 10,000 wamefariki mjini Tacloban na kwingineko.Mamia ya wengine wamepoteza makao yao.

Kimbunga hicho kimepiga Kaskazini mwa Vietnam karibu na mpaka na China , ingawa kasi yake imepungua.

Katika eneo la kati mwa Ufilipino, manusura wa kimbunga kibaya kuwahi kushuhudiwa wamekuwa wakikusanya masalaio ya makaazi yao na wakiomba msaada wa chakula na dawa.

Kimbunga Haiyan kinasemekana kuwaua maelfu ya watu katika mji mmoja pekee,Tacloban

Mwandishi wa BBC katika eneo hilo ameielezea hali kuwa mbaya kukiwa hakuna majengo yaliosalia , matope kila mahali, mifugo waliofariki na harufu ya miili iliyooza.

Katika kisiwa jirani cha Cebu, afisa moja alisema asilimia themanini ya baadhi ya miji huko kaskazini iliharibiwa.

Shughuli za uokozi zinaathirika kwa kuwa barabara na daraja zimeharibika. Balozi wa Uingereza nchini humo Ufilipino Asif Ahmad amesema ni janga lenye athari kubwa mno na limetokea katika maeneo maskini ya nchi hiyo.