Kenya iwe makini na wachezaji wake

Image caption Kenya imetakiwa kuwa makini na wachezaji wake wanaodaiwa kutumia dawa za kusisimua misuli

Rais wa shirika la kupambana dhidi ya dawa za kusisimua misuli john Fahey ameiambia BBC kwamba shirika lake halina nguvu za kukabiliana na mataifa pamoja na mashirika ya michezo ambayo uwezo wake wa kupima dawa hizo ni wa viwango vya chini.

Bwana Fahey amesema kuwa mpango wote wa kupima dawa za kusisimua misuli miongoni mwa wanariadha ni jambo la hiari na hivyo basi ni wajibu wa mataifa kama vile Kenya na Jamaica yenye wanariadha mahiri kufanya uchunguzi mwafaka.

Kiongozi huyo alikuwa akizungumza kabla ya kuanza kwa mkutano wa kupigana dhidi ya dawa za kusisimua misuli nchini Afrika kusini hii leo.

wajumbe watajadiliana kuhusu rasimu ya pendekezo la kuongeza marufuku kwa washukiwa wa dawa hizo toka kwa miaka 2 hadi miaka minne.