Boko Haram kutajwa kuwa kundi la kigaidi

Image caption wapiganaji wa kundi la Boko Haram la Nigeria

Marekani inataraji kutangaza rasmi kulitambua kundi la wapiganaji wa kiislamu la Boko kama kundi la kimataifa la ugaidi . Uamuzi huo umechukuliwa leo ambapo idara za usalama za marekani zimeelekezwa kukata mitandao ya kibiashara ya kundi hilo pamoja na njia zote za usafirishaji fedha ili kudhibiti kupanuka kimataifa

Hatua hii itaiwezesha Marekani pia kwa mjibu wa sheria ya taifa hilo kutolisaidia hilo la Kiislam ambapo lipo katika harakati za lazimisha kuwepo kwa sharia ya kutambulika kwake huko kaskazini mwa Nigeria.

Pamoja na kundi hilo kuwepo zaidi nchini Nigeria lakini Marekani inasema limekuwa likishirikiana na mtandao wa kimataifa wa Ugaidi wa Al Qaeda ambapo matawi yake yapo pia Afrika Magharibi na pia nchini Mali

Marekani haijalitambulisha rasmi kundi hilo kama la kigaidi japo kuwa taarifa za mashirika ya habari yanaarifiwa kuwepo kwa mpango huo wa marekani dhidi ya kundi la Boko Haram.

Kundi hili la Boko Haram lilianzishwa mwaka 2009 huku mashambulizi yake yakielekezwa katika vituo vya jeshi,katika shule na kuendesha mapigano na vikosi vya ulinzi nchini Nigeria.

Mchambuzi wa BBC nchini Nigeria Naziru Mikailu amesema uamuzi huo wa Marekani dhidi ya Boko Haram huenda ukapokelewa kwa furaha na na serikali ya Nigeria na taasisi za kikristo ambazo kwa muda mrefu zimekuwa zikilengwa na mashambulizi ya kundi hilo