Wafuasi wa Mohammed Morsi wafungwa

Image caption Wafuasi wa Mohammed Morsi wakiandamana

Mahakama moja nchini Misri imewahukumu wafuasi 12 wa rais aliyeng'olewa madarakani, Mohamed Morsi, kifungo cha miaka kumi na saba jela kila mmoja kwa kushiriki katika ghasia za mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu.

Watu hao walipatikana na hatia katika mashitaka kadha yakiwemo ya kufanya mashambulio na uhujumu uchumi, vitendo vilivyofanyika wakati wa maandamano yaliyoongozwa na wanafunzi katika taasisi ya elimu ya juu ya taasisi ya madhehebu ya Kiislam ya Sunni, Al-Azhar.