Boko Haram, Ansaru ni magaidi

Serikali ya Marekani imeweka makundi ya wapiganji wa Kiislam ya Boko Haram na lile la Ansaru katika orodha yake ya ugaidi .kutokana na sheria za Marekani sasa itakuwa kosa la jinai kutoa msaada wowote kwa makundi hayo yanayotuhumiwa kusababisha vifo vya watu wengi nchini Nigeria.

Marekani imesisitiza kuwa hii ni hatua mhimu katika kuisaidia Nigeria na mashambulizi kutoka katika makundi hayo mawali na kwamba sasa yatambulike kama makundi ya kigaid kama ilivyo kwa Al Qaeda.

Kutokana na hatua hiyo ya Marekani idara zake zinapaswa kusitisha biashara zote zinazoendeshwa mtandao huo wa kigaidi na kudhibiti usafirishaji wa fedha ndani ya makundi hayo

Pamoja na kundi hilo kuwepo zaidi nchini Nigeria lakini Marekani inasema limekuwa likishirikiana na mtandao wa kimataifa wa Ugaidi wa Al Qaeda ambapo matawi yake yapo pia Afrika Magharibi na Mali

Kundi hili la Boko Haram lilianzishwa mwaka 2009 huku mashambulizi yake yakielekezwa katika vituo vya jeshi,katika shule na kuendesha mapigano na vikosi vya ulinzi nchini Nigeria.