Mkutano wa Jumuiya ya madola Sri Lanka

Image caption Maandamano kupinga mkutano huo kufanyika Sri Lanka

Mkutano wa viongozi wa nchi wanachama wa jumuiaya ya madola, umeanza nchini Sri Lanka, lakini mkutano huo umegubikwa na mjadala mkali ikiwa ilikuwa sawa kuandaa mkutano huo nchini humo.

Canada, India na Mauritius wamesusia mkutano huo wakilalamika kuwa serikali ya Sri Lanka ilikataa kuchunguza madai ya ukikuwaji wa haki za binadamu wakati serikali ilipokuwa inapambana na waasi wa Tamil Tigers na kushinda mwaka 2009.

Rais Mahinda Rajapaksa amewashukuru watu waliohudhuria mkutano huo na kuinga mkono nchi yake.

Waziri mkuu wa Uingeza anahudhuria mkutano huo, lakini atafanya ziara nyingine hadi maeneo la kaskazini mwa Sri Lanka kukutana na viongozi wa Tamil ili kuelezea wasi wasi wake.

Warsha hiyo imefunguliwa huku mwana mfalme Prince Charles,akimwakilisha mama yake Malkia Elizabeth, kama mkuu wa Jumuiya ya Madola .

Mkutano huu umeanza kuhusu mkutano mwingine uliokuwa unaangazia haki za binadamu mjini Colombo ukifungwa na maafisa wakuu nchini humo.

Mkutano huo hata hivyo ulitarajiwa kufungwa. Mnamo Jumatano na Alhamisi mkutano huo ulivamiwa na makundi yanayounga Serikali mkono, kukiwemo na watawa wa Kibudha na hali hiyo ilitokea baada ya muda Polisi kuamuru kuwa mkutano huo ufungwe.

Tayari maafisa wa usalama Kaskazini mwa Siri Lanka walikuwa wamezuia mabasi yaliyokuwa yamewabeba watu wa kabila la Watamil kuelekea Colombo kwa mkutano huo wa Haki za Kibinadamu.

Mashirika ya kiraia kwa wakati huu yanajitahidi kadiri ya uwezo wao kujaribu kupata habari kuwahusu maelfu ya watu waliotoweka; wengine wao kuanzia mwaka 1990.

Hadi kufikia sasa Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, pamoja na mwana Mfalme wa Uingereza, Prince Charles, wamefika nchini Sri Lank kuhudhuria mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya Madola. Prince Charles atafungua rasmi mkutano huo akimwakilisha mamake, Malkia Elizabeth wa Uingereza.

Siku chache zilizopita Bwana Cameron na viongozi kadhaa wa Sri Lanka wamekuwa wakijibizana vikali kufuatia tangazo la Bwana Cameron kuwa atazua mjadala wa hali mbovu ya haki za kibinadamu nchini Sri Lanka. Lakini viongozi wa Sri Lanka wamesema kuwa hawatamruhusu kuzusha mjadala huo ambao Serikali hiyo, mwenyeji wa mkutano huo inaona kama ni madharau.

Bwana Cameron ametetea ziara yake ya Sri Lanka, licha ya makundi kadhaa kumshauri aususie mkutano huo kwa sababu za ukiukaji wa haki za kibinadamu wa taifa hilo. Kwa upande wake Cameron amesema ukiukaji huo ambapo wanajeshi waliwatendea unyama waasi wa Tamil Tiger ni swala ambalo lazima alizungumzie.

Waziri Mkuu huyo wa Uingereza alisisitiza kuwa ni heri ajitokeze na kuangazia swala hilo akiwa mkutanoni ngambo badala ya kukaa nyumbani.

Mkereketwa wa Haki za Kibinadamu wa Sri Lanka, Brito Fernando, amesema kuwa jamii ya kimataifa inapaswa kupida darubini kwa yote yanayoendelea nchini Sri Lanka.