Mtunzi wa riwaya Doris Lessing afariki

Doris Lessing na tuzo ya Nobel mwaka wa 2007

Mwandishi wa riwaya aliyewahi kupata tuzo ya Nobel, Doris Lessing, amefariki akiwa na umri wa miaka 94.

Alizaliwa Persia, yaani Iran, na alikulia Rhodesia Kusini, yaani Zimbabwe, kabla ya kuhamia London ambako ndiko alikofariki.

Ameandika vitabu zaidi ya 60, kati yao ni The Grass Is Singing na The Golden Notebook, akitazama maswala mbali-mbali pamoja na ukoministi, ukabila na tofauti baina ya wanawake na wanaume.

Alipata Nobel akiwa na umri wa miaka 88 mwaka wa 2007, na kuwa mwandishi mzee kabisa kuwahi kupewa tuzo hiyo.