Ubalozi wa Iran washambuliwa Beirut

Image caption Mlipuko karibu na ubalozi wa Iran, mjini Beirut, Lebanon

Watu wapatao 22 wameripotiwa kuuawa katika milipuko miwili ambayo imepiga mfululizo karibu na ubalozi wa Iran katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut.

Afisa ubalozi wa Iran Ebrahim Ansari ni miongoni mwa waliouawa katika milipuko hiyo. Maafisa wamesema idadi ya waliokufa inaweza kuongezeka.

Picha za televisheni zimeonyesha magari yakiungua, maiti zikiwa zimelala mtaani na majengo yaliyoharibiwa.

Iran imekuwa ikikiunga mkono kikundi cha Hezbollah ambacho ni cha wapiganaji wa madhehebu ya Kiislam ya Shia, ambacho kimetuma wapiganaji wake kwenda Syria kusaidia serikali ya Rais Bashar al-Assad.