Pambaja lawatia mashakani Saudia

Image caption Polisi wa kidini waliwakamata wawili hao na kuwaonya

Wanaume wawili wamekamatwa nchini Saudi Arabia kwa kuwapa pambaja wapita njia mjini Riyadh.

Maafisa wakuu nchini humo wanasema kuwa polisi waliwazuia wanaume hao kwa kuhusika na vitendo visivyokubalika na kuleta kero kwa umma.

Waliweka video kwenye mtandao ikiwaonysha wakiwapa pambaja watu wasiowajua ambao walikuwa wanaume pekee wala sio wanawake.

Video hiyo imetazamwa na zaidi ya watu milioni moja.

Polisi wa kidini waliwalazimisha kutia saini makubaliano kuwa hawatafanya hivyo tena.

Watu nchini Saudia wamekuwa na maoni tofauti kuhusu kitendo cha wanaume hao.