Washukiwa wa ugaidi kususia chakula Uganda

Image caption Washukiwa hao wanazuiliwa katika gereza la Luzira

Washukiwa kumi na wawili wa shambulizi la kigaidi lililofanyika nchini Uganda mwaka 2010 wametishia kuanza kususia chakula kama ishara ya kulalamikia kucheleweshwa kwa kesi zao.

Kumi na wawili hao wakiwemo wakenya sita ,wamekuwa wakizuiliwa Uganda tangu mwaka 2011 baada ya kuhusishwa na shambulizi la mabomu dhidi ya mkahawa mmoja nchini wakati wa fainali ya kombe la dunia mwaka huo nchini Afrika Kusini.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa shirika la kuteteta haki za waisilmu, la Muslim Human Rights Forum (MHRF), Al-Amin Kimathi, wale waliotishia kuwa watagoma kula ni pamoja na Omar Awadh Omar, Idris Magondu, Habib Suleiman Njoroge, Hussein Hassan Agade, Yahya Suleiman Mbuthia na Mohamed Ali Mohamed.

"kumi na wawili hao wamewasilisha onyo lao la kuanza kususia chakula kuanzia Jumatatu,'' alinukuliwa akisema bwana Kimathi.

Al -Amin Kimathi amekuwa akifutialia kesi hiyo tangu ilipoanza mwaka huo na mwenyewe alizuiliwa na washukiwa hao baada ya kwenda Uganda kujaribu kupinga kukamatwa kwa washukiwa hao.

Kimathi alisema kuwa watu hao wamezuiliwa katika jela ya Luzira na wanalalamika kujikokota kwa kesi yao ambayo ilianza mwaka 2011 tangu waliposhitakiwa rasmi.

Wanaume hao wamekuwa wakizuiliwa tangu mwaka 2011 wakisubiri kusikilizwa kwa ombi lao la kikatiba walilowasilisha katika mahakama ya kikatiba ya Uganda Septemba mwaka 2011.

Hata hivyo kuchelewa kwa kesi yao kunatokana na Ombi hilo walilowasilisha hali iliyolazimu kesi dhidi yao kuahirishwa.

Washukiwa hao, waganda wanne, mkenya mmoja na mtanzania mmoja pamoja na wakenya sita wanailaumu serikali ya Uganda kwa kuchelewesha kesi yao bila sababu kuhakikisha tu kuwa wanazuiliwa bila kusikilizwa kwa kesi yao.

Wanadai kuwa juhudi zao za kutaka kesi isikilizwe na kuamuliwa haraka, zimetatizwa na serikali.

Bwana Kimatyhjio ambaye amekuwa akifuatilia kesi hiyi tangu ilipowasilishwa mahakamani, amesema kuwa hatua inayochukuliwa na wafungwa ni kitendo cha kuonyehs akuwa sreikal zao zimewapuuza huku Uganda ikiechelesha kesi hizo bila ya sababu hali inayotokana na serikali yenyewe kutokuwa na ushahidi.