Ndege za washirika zapita anga ya China

Image caption Ndege ya Japan

Japan na Korea Kusini zimerusha ndege za kivita kupitia eneo jipya la ulinzi wa anga lililowekwa na China katika kile kinachoonekana kuwa jaribio la kuona ambavyo China amedhibiti eneo hilo la anga.

Habari hizo zimekuja baada ya Marekani kurusha ndege mbili za kivita aina ya B-52 kupitia anga hiyo, iliyopo katika visiwa vinavyozozaniwa Mashariki mwa Bahari ya China.Si Japan, Korea Kusini wala Marekani iliyoiarifu China kuhusu urushaji wa ndege zao za kivita katika eneo hilo-- kama China inavyotaka sasa.

Nchi nyingi zimeishutumu China kwa uamuzi huo wa kutenga eneo la ulinzi wa anga , zikisema kwamba hilo ni jaribio la kutaka kubadili uwiano wa nguvu za kijeshi kwa lazima.