Shinawatra apona kuondolewa madarakani

Image caption Yingluck Shinawatra,waziri mkuu Thailand

Waziri Mkuu wa Thailand, Yingluck Shinawatra, amepona kung'olewa madarakani baada ya kushinda kura ya kutokuwa na imani naye.

Kumekuwa na maandamano siku kadhaa kutaka waziri mkuu huyo ajiuzulu kwa madai kwamba ni kibaraka wa waziri mkuu wa zamani Tasin Shinawatra ambaye ni kaka yake na waziri mkuu Yingluck.

Ameshinda kirahisi kwa kupata idadi kubwa ya kura alizohitaji kutoka baraza la chini la bunge la nchi hiyo, ambalo wajumbe wake wengi ni kutoka muungano wa chama chake.

Waandamanaji ambao walizingira majengo ya wizara kadha mjini Bangkok wamesema watasitisha kwa muda maandamano yao.

Wanasema lengo lao ni kuondoa mfumo mzima wa siasa kwa sababu wanafikiri mfumo huo umehodhiwa na kaka yake waziri mkuu Yingluck, Taksin Shinawatra ambaye anaishi uhamishoni.