Abiria wote ndege ya Msumbiji wamekufa

Ndege ya shirika la ndege la Msumbiji ambayo ilikuwa imepotea nchini Namibia imepatikana japo abiria wote 34 waliokuwa wamepanda ndege wote wamepoteza maisha maafisa wa polisi wasema.

Ndege hiyo iliyokuwa imeungua imepatika kwenye mbuga ya wanyama Bwabwaata karibu na mpaka wa Angola na Botswana.

"Ndege imeteketea yote yamebaki majivu tu hakuna hata mtu mmoja aliyenusurika," Naibu Kamishna wa Polisi nchini Namibia Willy Bampton amenukuliwa na shirika la habari la Reuters.

Ndege hiyo namba TM470 iliondoka Maputo nchini msumbiji tangu siku ya ijumaa na ilikuwa ikielekea Luanda chini Angola.

Inaelezwa kuwa masiliano ya mwisho na ndege hiyo ilikuwa ni wakati ilipofika kaskazini mwa Namibia.

Kwa mujibvu wa shirika la ndege la Msumbiji abiria walipanda ndege hiyo ni raia 10 wa Msumbiji, Angola 9, Wareno 5, Mfaransa 1 , Mbrazili 1 na Mchini 1.