Mashabiki watetemesha ardhi US

Shangwe na hoi hoi za mashabiki wa mchezo wa American football katika mji wa Seattle nchini Marekani zilisababisha kishindo kikubwa cha makelele kusababisha tetemeko dogo la ardhi,kwa mujibu wa wanasayansi.

Mashabiki waliokuwa waliokuwa na furaha waliruka huku na huko lilipofungwa bao la mapema katika mchezo kati ya Seattle Seahawks na New Orleans Saints.

Kituo kinachochunguza na kupima mitetemeko ya ardhi The Pacific Northwest Seismic Network kilibaini mtikisiko wa vipimo baina ya 1 na 2 ya nguvu za tetemeko la ardhi.

Seahawks walishinda mchezo huo katika uwanja wa CenturyLink Field kwa pointi 34-7.

Mkurugenzi wa kituo cha Pacific Northwest Seismic Network John Vidale aliiambia CNN kwamba wanasayansi wake walirikodi mitikisiko 5 tofauti ya ardhi wakati wa mchezo huo.

Hii si mara ya kwanza; kwani mwaka 2011 mashabiki wanaoshangilia walisababisha ardhi ya Seattle kutikisika katika mchezo mwingine wa American Football.

Uwanja wa CenturyLink Field, ambao ni wazi pia uliweka rekodi ya dunia ya takwimu za Guinness World Record