Mwalimu Mmarekani auawa Libya

Image caption Mji wa Benghazi umekuwa ukikumbwa na vurugu za mara kwa mara tangu Gadafi kuondolewa mamlakani

Mwalimu anayeaminika kuwa raia wa Marekani ameuawa kwa kupigwa risasi mjini Benghazi Mashariki mwa Libya.

Maafisa wanasema kua mwalimu huyo kutoka mjini Texas Marekani, alifundisha somo la Kemia katika shule moja ya kimataifa.

Mwanamume huyo anayesemekana kuitwa Ronnie Smith, anasemekana kupigwa risasi alipokuwa anafanya mazoezi katika mtaa wa Fweihat.

Hata hivyo ubalozi wa Marekani haujatoa taarifa yoyote kuhusiana na mauaji hayo.

Pia hakuna kundi lililojitokeza kuhusika na mauaji hayo.

Shule ya kimataifa alikokuwa anafunza mwalimu huyo, sio ya kimarekani, bali inafuata mfumo wa shule za Marekani.